May 8, 2016

RWEYMAMU
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Soka Manispaa ya Kinondoni (KIfa), umevurugika katika hatua za mwisho kabisa.

Uchaguzi huo ambao umefanyika katika Ukumbi wa Mbezi Rest katika eneo la Mbezi jijini Dar es Salaam, umevurugika baada ya kugundulika kulikuwa na kura zilizoongezeka.

Hilo limegundulika usiku huu kuanzia muda wa saa 4:30 usiku, wakati wapiga kura waliingia ukumbini saa 2:30 asubuhi.

Wakati uchaguzi unavurugika, Salum Mwaking’inda alikuwa anaongoza kwa kura akionekana kumzidi kwa karibu mpinzani wake Patrick Rweymamu ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa kwa kuwa alionekana ni chaguo la vijana na wadau wengi waliotaka maendeleo ya mchezo wa soka katika Manispaa ya Kinondoni.

Hata hivyo, baadaye iligundulika kulikuwa na ongezeko la kura mbili ambazo hazikujulikana zilitokea wapi.

Kwani mkanganyiko ulianza mapema baada ya kutangazwa kuna jumla ya kura 209 zitakazopigwa. Lakini baada ya utulivu na marudio ikaonekana jumla ni kura 216.

Lakini baada ya zoezi la upigaji kura, zilipojumlishwa pamoja na Mwaking’inda kuonekana ana nyingi zaidi ya Rweymamu, lakini jumla ikawa kura 218.

Baada ya hapo mzozo ukaanza na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi, Samwel Ntaliba akaona kweli kuna tatizo na kusema kikubwa ni uchaguzi urudiwe ili kuondoa figisu hizo.

Kauli hiyo ilionekana kuwaudhi baadhi hasa wanaoonekana kumuunga mkono Mwaking’inda, vurugu zikaanza na viti vikarushwa kama tiara.


Taarifa za mwisho zinaeleza kwamba uchaguzi huo utapangiwa tarehe lakini imekuwa kazi kubwa kupata uhakika wa mambo mengine kwa kuwa eneo hilo halikuwa limetulia.

Salehjembe.blogspot.com

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic