May 1, 2016


Maisha ni hatua, mshambuliaji Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini hajaonekana uwanjani zaidi ya mwezi sasa.

Mashabiki wa soka wamekuwa wakitaka kujua vipi au nini tatizo huku wengine wakiamini ameisha.


Lakini Ngassa amezungumza na SALEHJEMBE kutoka nchini Afrika Kusini na kuelezea namna ambavyo mambo hayakuwa mazuri baada ya kuumia goti na kufanyiwa upasuaji.

“Watu wengi hawakuwa wamelijua hili. Niliumia goti nikalazimika kufanyiwa upasuaji. Nilikuwa nikitembea kwenye kiti cha matairi.

“Baadaye nilirejea katika hali ya kawaida hata hivyo bado kidogo. Hivyo hili ndilo lililonikuta hadi kukaa nje,” alisema.

Watanzania wengi walikuwa wakishangazwa kutomuona Ngassa hata benchi kila Free State Star ilipokuwa ikicheza.

Jambo ambalo lilizua mjadala na Ngassa ameeleza hilo na tunatarajia kumpata kesho ili atueleze zaidi na anaendelea kwa sasa na nini anachokifanya.

Ngassa amejiunga na kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini akitokea Yanga na moja kwa moja akafanikiwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV