November 5, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa anafurahishwa na namna wachezaji wake wanavyojituma wakiwa uwanjani, makosa ambayo wanayafanya ni ya kiufundi anayafanyia kazi.

Mgunda amesema kuwa mchezo wa mpira hauhitaji papara hasa katika kutafuta matokeo bali ni umakini na mbinu kwa wachezaji kuhakikisha wanafanikiwa kupata matokeo.


"Wachezaji wanajituma, linapokuja suala la matokeo huwezi kutabiri kwa sababu mpira ni dakika 90, ila najivunia uwepo wao uwanjani kwa kuwa wanapambana kuhakikisha wanapata matokeo hivyo maandalizi yetu  kwa ajili ya mchezo huanza baada ya kumaliza mechi moja," alisema.


Coastal wamefanikiwa kucheza michezo 13 mpaka sasa na kujikusanyia pointi 19 ambazo zimewafanya wawe kwenye nafasi ya tano ikiwa ni timu ya kwanza kwa zile ambazo zimepanda daraja msimu huu, mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Ndanda FC uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic