July 19, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya Azam upo kwenye mipango ya kupitisha panga kubwa ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kufanya maboresho ya kushusha nyota wapya na kuachana na baadhi ya waliopo ambao hawakutoa mchango uliostahili.

 

Azam imepata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao baada ya kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

 

Katika michuano hiyo msimu ujao, Azam itakuwa sambamba na Biashara United iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo, huku mabingwa Simba na Yanga wakipata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Azam, Vivier Bahati, alisema: “Kwanza tunajivunia sana nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao. Haya ni mafanikio ya malengo yetu kwa msimu huu.

 

“Kuelekea michuano hiyo, tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri na ni lazima tuandae kikosi kitakachokuwa imara kwa ajili ya kuweka heshima, hivyo tunatarajia kufanya usajili wa maboresho katika maeneo ambayo tunadhani yana mapungufu.

 

"Katika mpango huo, tutaachana na baadhi ya wachezaji ambao tunadhani hawakuwa na mchango ambao tulikuwa tunafikiria," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic