May 6, 2016


Mshambuliaji nyota wa Leicester City, Jamie Vardy ameongeza tatuu nyingine kwenye mwili wake.

Vardy ameongeza tatuu hiyo ikiwa ni muds mchache kabla ya kikosi chake kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya Chelsea kuibana Tottenham na kutoka nayo sare ya mabao 2-2.

Straika huyo alichora tatuu yake katika sehemu maalum inayomilikiwa na Nik Moss-Glennon ambaye ni mchora tatuu mahiri zaidi.


Baada ya mashabiki wa Leicester kugundua kwamba Vardy alikwenda pale na kuchora tatuu inayoelezwa ilitumia saa saba. Nao wameweka oda kwa wingi wakitaka kwenda eneo hilo na kujichora pia na tayari wameanza kuchorwa na mtaalamu huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV