May 28, 2016

Baraza la wazee la Yanga wameliomba Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwakubalia kutumia kadi mbili za zamani na za Posta katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.


Uchaguzi mkuu wa Yanga umepangwa kufanyika Mei 27, mwaka huu na Kamati ya TFF imetangaza uchaguzi huo juzi ilitangaza jana ndiyo siku ya kuanza kutoa fomu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa baraza la wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amesema kama kuna baadhi watapiga kura na wengine kuachwa, haitakuwa sawasawa.

"Kama wengine watapiga wakiwa na kadi za zamani ana kuwaacha wale wenye kadi za uanachama za benki ya Posta, haitakuwa sawa.

"Wako waliokuwa wana kadi za zamani, wakabadili na kuchukua zile za Posta. Wengine kweli ni wapya, sasa kuwaacha wengine na wengine wapige ni kuleta mgogoro," alisema Akilimali.


Pia baraza hilo limeomba BMT na TFF kuitishwa mkutano wa dharura wa klabu hiyo ambao utahusiana na masuala ya uchaguzi.

"Pia ninaomba kama watakubali katika mkutano huo pia wawashirikishe watu kutoka wizara ya michezo, viongozi wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA)," alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV