May 28, 2016Klabu ya Genk ya Ubelgiji imesema itamwachia Mbwana Samatta Juni Mosi ili kuja nchini kujiunga na Taifa Stars lakini si kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya.

Hali kadhalika, TP Mazembe nayo imekataa kumuachia Thomas Ulimwengu kwa ajili ya mechi hiyo kwa kuwa ina majukumu muhimu.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amethibitisha hilo kuwa TP Mazembe itaivaa AS Vita katika mechi yenye upinzani mkubwa.

“Kweli hilo limethibitishwa na Mazembe kuwa wana majukumu muhimu ikiwemo mechi hiyo dhidi ya AS Vita ambayo kwao ni mechi ya upinzani mkubwa,” alisema Alfred.


Stars iko nchini Kenya kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wake Harambee Stars ikiwa ni maandalizi ya kuivaa Misri jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV