June 14, 2016Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali amesema baada ya uchaguzi, Wanayanga wavunje makundi.

Akizungumza ma SALEHJEMBE, Akilimali amesema ni vizuri makundi yavunjwe kama yalikuwepo ili waungana.

“Tunaweza kuungana sasa, uchaguzi umepita na kama watu wote wawe pamoja kabisa ili tuisaidie klabu yetu, makundi hayatatusaidia lolote,” alisema.


Yanga imepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV