June 14, 2016

Beki wa kati wa Yanga, Vicent Bossou anaondoka usiku wa kuamkia kesho kwenda Antalya nchini Uturuki kuungana na wenzake.

Bossou atapitia jijini Istanbul kwenda Antalya ambako Yanga imeweka kambi kujiandaa na Mo Bejaia katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tayari Bossou lifika klabuni, amekabidhiwa tiketi na kila kitu safi anaondoka kwenda Uturuki,” kilieleza chanzo.


Beki huyo raia wa Togo, alikuwa nchini Ivory Coast ambako inaelezwa alibanwa na matatizo ya kifamilia. Kiasili anatokea nchini Ivory Coast.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV