June 4, 2016


Baada ya Yanga kumsajili beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy, Mrundi, Karim Nzigiyimana wa Gor Mahia amesema yupo tayari kutua Msimbazi kuchukua nafasi ya Kessy.

Kama ilivyo kwa Kessy, Nzigiyimana naye anamudu kucheza nafasi ya beki wa kulia na anasisitiza kamwe Simba haitajuta ikimsajili. 

Nzigiyimana ambaye ni kiraka mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani isipokuwa langoni, alijiunga na Gor Mahia mwaka 2011 akitokea Rayon Sport ya Rwanda.

 Akizungumza kutoka kutoka Burundi, Nzigiyimana alisema, amesikia Kessy ameondoka Simba, hivyo anataka kuchukua nafasi yake ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kucheza soka Tanzania. 

“Nimesikia Kessy ameondoka Simba sasa nipo tayari kuja kuchukua nafasi yake kwa sababu nimebakisha mkataba wa miezi sita na Gor Mahia, Kessy ni mchezaji mzuri ambaye tunafanana katika kucheza  sasa naamini kama Simba wakinifuata itakuwa vizuri.

“Sijazungumza na Gor Mahia hadi sasa kwani nadhani umefika wakati wa kucheza nje ya Kenya na chaguo langu la kwanza ni Tanzania na kwa kuwa Simba imeachana na Kessy, nataka kwenda hapo,” alisema Nzigiyimana.

Beki huyo alisema anaamini ligi ya Tanzania ni bora na atacheza kwa ushindani mkubwa endapo atapata nafasi ya kucheza Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic