June 4, 2016


Bondia Cosmas Cheka, leo Jumamosi anatarajia kupanda ulingoni kugombea Mkanda wa Ubingwa wa Dunia (UBO) kupambana na Mmalawi, Chrispin Moliyati kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar.

Promota wa pambano hilo la raundi 12, Juma Ndambile, alisema licha ya kuwepo kwa pambano hilo la ubingwa, lakini pia kutakuwa na mapambano mengine yatakayokuwa na upinzani mkali.


 “Maandalizi yamekamilika na Cosmas atapambana na Moliyati lakini pia Japhet Kaseba atacheza na Amour Mzungu, Alphonce Mchumia Tumbo atapigana na Mussa Ajibu wa Malawi na pia kutakuwa na mapambano mengine mengi,” alisema Ndambile.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV