June 11, 2016Beki wa kati wa Yanga, Mtogo, Vincent Bossou, ndiye mchezaji pekee wa kimataifa wa timu hiyo ambaye hajajiunga na kikosi hicho kinachojiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bajaia ya Algeria.

Hali hiyo imesababisha wasiwasi kwa baadhi ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo ambao tayari wanamwamini beki huyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa msimu uliopita.

Hata hivyo, Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh ameliambia Championi Jumamosi kuwa mchezaji huyo alichelewa kutua nchini kutokana na kukwama nchini Ivory Coast kwa matatizo ya kifamilia.

“Bossou amechelewa kutua hapa nchini kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia huko kwao Ivory Coast, lakini kesho (leo) anatarajia kuwasili.

“Najua utajiliuza  kuhusiana na Ivory Coast. Lakini mchezaji huyo kwao ni Ivory Coast ila Togo alichukua uraia tu wa nchi hiyo kama ilivyo kwa Mbuyu Twite ambaye ni Mkongo ila ana uraia wa Rwanda,” alisema Hafidhi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV