June 14, 2016


Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ufundi ya Simba, wamegoma katakakata kuona kiungo Haruna Chanongo anarejea Msimbazi.

Wajumbe hao na baadhi wa kamati ya usajili, wameonekana kutofurahishwa na mjadala wa Chanongo ambaye anaelezwa ameomba kurejea Simba.

“Kaomba sana kwa kweli, lakini tumemkatalia. Kuna kiongozi mmoja ana nia nzuri na ana imani atakuwa ni mtu aliyebadilika.

“Lakini wengi tumekataa, Chanongo aliondoka na maneno mengi, dharau na alionyesha wazi hakuwa anashida na Simba. Sasa kakataliwa Yanga, ndiyo anataka kurudi! Hapana kabisa,” kilieleza chanzo.

Lakini taarifa nyingine zinaeleza kwamba bado suala hilo liko kwenye mjadala na inawezekana Chanongo akarejea kwa kuwa ndiye amekuwa akiomba na ameahidi atapambana “kwelikweli”.

Chanongo sasa anaichezea Stand United ya Shinyanga ingawa amekuwa hana uhusiano mzuri ana Kocha Patrick Lieiwig ambaye alikuwa kocha wake akiwa Simba.


Hivi karibuni, alipata nafasi ya kufanya majaribio katika kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo lakini akafeli na kurejea Stand United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV