June 14, 2016

AFRICAN SPORTS


Tayari makundi ya Ligi Kuu Daraja la kwanza yametoka na inaonyesha ni nafasi nyingine kwa timu za Tanga kurejea Ligi Kuu Bara.

Msimu wa 2015-16 umemalizika kwa aibu kubwa mkoani Tanga baada ya timu zote tatu zilizokuwa Ligi Kuu Bara kuteremka daraja.

Coastal Union ndiyo liana, ikafuatiwa na African Sports na baadaye Mgambo Shooting, hivyo kuifanya Tanga kuweka rekodi hiyo mbaya.

Kwa kuwa timu zake ziko kwenye makundi matatu tofauti ya A ambako wako African Sports, B wako Coastal Union na Mgambo wamepangwa C. Maana yake ni nafasi nzuri kwao kwa kuwa hawatakutana na inakuwa ni kazi rahisi kusaidiana kwa vile kila mmoja yuko upande mwingine.

Kundi A:
1        Abajalo ya Dar es Salaam
2        African Sports ya Tanga
3        Ashanti United       ya Dar es Salaam
4        Kiluvya United ya Pwani
5        Friends Rangers ya Dar es Salaam                 
6        Lipuli  ya Iringa               
7        Mshikamano FC ya Dar es Salaam         
8        Polisi Dar ya Dar es Salaam
                 
Kundi B:
1        JKT Mlale ya Ruvuma
2        Coastal Union ya Tanga
3        Kimondo FC ya Mbeya
4        Kinondoni Municipal Council      ya Dar es Salaam
5        Kurugenzi     ya Iringa
6        Mbeya Warriors ya Mbeya
7        Njombe Mji  ya Njombe
8        Polisi Morogoro      ya Morogoro

Kundi C:
1        Alliance Schools ya          Mwanza
2        Mgambo Shooting   ya Tanga
3        Mvuvumwa FC ya    Kigoma
4        Panone FC ya Kilimanjaro
5        Polisi Dodoma        ya Dodoma
6        Polisi Mara   ya Mara
7        Rhino Rangers        ya Tabora

8         Singida United ya Singida

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV