June 17, 2016Mshambuliaji Obey Chirwa wa Platinum FC ya Zimbabwe amekubali kutua Yanga.

Mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Omese Mwani akisema anasimamia masuala yake ya usajili, amesema akitua leo nchini, litakuwa ni suala la kusaini mikataba tu.

“Kweli mwanzo kulikuwa na shida kidogo, lakini hadi Chirwa anakuja huko Tanzania maana yake amekubali. Kama kila kitu kitakwenda sawa, atasaini mataba.

“Anakuja huko leo, hivyo acha tuone mambo ya mwisho yanakuwa vipi halafu tutawaambia,” alisema.


Yanga ilianza kusaka wachezaji mbalimbali lakini mwisho imeangukia kwa Chirwa raia wa Zambia ambaye anaonekana kuivutia zaidi na wachezaji wamemkubali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV