June 4, 2016



Tuite nini fazaa? Taharuki? Nadhani tuliite pigo la ulimwengu. Sshujaa wa watu wote na mfalme mwema Muhammad Ali ametutoka ghafla leo huko Scottsdale Arizona leo tarehe 4 June 2016.

Nimeita pigo kwa sababu king Ali alikuwa ni alama ya ustaarabu mpya duniani. Ustaraabu wa kuwatambua watu wa imani tofauti na wakaheshimiana, ustaraabu wa thamani ya mtu mweusi, ustaraabu wa kutumia sanaa ya michezo hususan fight. Kuwa ni kielelezo cha upendo, amani na mshikamano.


Najua washangaa kwa nini nimeanza na falsafa hizo ninazo sababu lakini niitaja kubwa moja huwa kila siku nasema michezo inaweza kuinganisha jamii iliyotengana. Michezo inaweza kuleta maji penye kiu michezo inaweza kuleta tiba penye maradhi, michezo inaweza kuleta amani penye vita na ndiyo maana king mwingine duniani Pele aliweza kusimamisha vita ya Biafra kule Nigeria. Pale klabu yake ya Santos ilipotembelea taifa hilo miaka ambayo vita ilikuwa ikipiganwa.

Ali ameleta kila kitu kupitia ngumi kaleta maji penye kiu kule Afghanistan. Kaleta amani penye vita kule Iraq na hata tiba penye maradhi kule Ethiopia 1983.

Ni nani king Ali?
Ni mfalme wa mchezo wa ngumi duniani ambaye hajapata kutokea ni mwanamiche muungwana zaid duniani kuwahi kutokea lakini ndio mwanamichezo bora wa karne iliopita akipambana mapambano 61 ya ngumi.akishinda 56 huku 37 akishinda kwa KO. Licha ya hayo king Ali ni mshindi wa medali ya dhahabu ya olimpiki kule Rome itali 1960, zama hzo akifight na uzito wa light heavy kabla ya kujiunga na ngumi za kulipwa ambako alipigana katika uzito wa heavyweight .

Bahati mbaya hii makala hii nilipanga iwe fupi ningekupa habari za mapambano yake maarufu hususan na Joe freizer na George foreman. Ila tambua dunia leo imempoteza shujaa wa watu wengi kama si wote.

Kuna wakati mzaliwa huyo wa Louisville Kentucky ambae alipewa jina la Cassius Marcellus Clay Jr na baadaye kusilimu kisha kutumia jina lake maaruf Muhammad Ali. Alipata kumdhalilisha kwenye ring bingwa wa zamani Liston kwa kumlazimisha amwite jina lake jipya Muhammad. 

Liston alikuwa hatambui imani mpya ya Alli. Na king akaamua kumlazimisha kumwita jina jipya ulingoni.....who's my name? Ali alisikika akimuuliza Liston ulingoni huku akitupa jeb jeb..liston hatimaye alilitamka jina hilo Ali.

Miaka yake 74 ulimwenguni ameacha alama kubwa sana na dunia haitamsahau kiumbe huyo aliyejaaliwa sura za kina nabii Yusuf.

Mungu mpokee people's champion Louisville RIP king of the kings....man of the century....
Nimehemewa na kuandika..chozi langu hili linanikumbusha msiba wa madiba...

Inna lillah wa inna ilaihi raajiun



Haji S.Manara

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic