June 17, 2016



Licha ya Azam FC kuwa kimya katika suala la usajili, imebainika kuwa tayari imeletewa beki wa kati kutoka Cameroon.

Imeelezwa kuwa beki huyo aliyefahamika kwa jina moja la Tuko, ameletwa na mmoja wa mawakala aliyependekeza kupelekwa Azam kwa ajili ya majaribio na kama Azam itamuelewa, basi aingie kandarasi na matajiri hao.

Mtu wa ndani kutoka klabuni hapo amesema kuwa, mchezaji huyo yupo nchini kwa takriban wiki mbili sasa na alitua kimyakimya na kutulizwa kwa ajili ya kusubiri kuanza kwa mazoezi ya timu hiyo na yeye aonyeshe kiwango chake.

“Unajua Tanzania sasa hivi hata kama utaletwa na wakala na kama timu haikujui, lazima wakuangalie kwanza kwa kukujaribu kabla ya kukusajili na sasa hivi ametulia, anasubiri kama mambo yataenda vizuri, timu ikianza mazoezi naye ajiunge kuangaliwa zaidi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, kuzungumzia hilo, ambapo alisema: “Hapana, utaratibu wetu hauendi hivyo, timu kwa sasa ipo mapumzikoni na hatujatangaza chochote kuhusiana na wachezaji wapya, siku ikifika tutawaambia na mtawaona mazoezini, hizo taarifa nyingine sisi hatuzijui."

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic