June 23, 2016


MBEYA CITY NA BIN SLUM WALIPOINGIA MKATABA WA KWANZA
Mbeya City inatarajia kupata mkataba mwingine kutoka kwa kampuni maarufu ya uuzaji matairi nchini ya Bin Slum Tyres kupitia betri zake imara za magari za RB.

Taarifa zinasema, huenda mkataba mpya kati ya Bin Slum na timu hiyo ya Mbeya, ukamalizika leo na kusainiwa.

“Kweli, leo linaweza kufanyika hilo suala. Bin Slum ni kampuni inayopenda kudhamini masuala ya michezo lakini inapenda kufanya kazi na watu wanaofanya mambo kwa weledi,” kilieleza chanzo.


Hatukufanikiwa kuwapata wahusika wa Bin Slum na tulielezwa walikuwa katika kikao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV