June 23, 2016Baada ya mvutano kati ya Yanga na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwamba mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe ichezwe lini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, sasa jibu ni Jumanna.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameendelea kusisitiza mechi hiyo itachezwa Jumanne kama ilivyotangazwa awali, na si kama walivyotangaza Yanga kuwa ni Jumanne.
Lakini Yanga kupitia Kurugenzi yao ya Habari na Mawasiliano, Msemaji wao, Jerry Muro amesema: “Ni kweli.”

Muro amesema wamefikia hivyo baada ya kutokuwa na uhakika kama kweli kuna umeme wa uhakika.

“Mechi itachezwa Jumanne na si Jumatano, kuchezwa usiku inaonekana hatuna uhakika wa umeme,” alisema Muro.


“Pia hatuna uhakika wa jenereta, hivyo hatuwezi kuingia kwenye hasara au kujaribisha kitu cha hatari wakati tunajua tunaweza kupoteza pointi kwa kanuni za Caf.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV