June 23, 2016

OMOG
Kocha Mghana, Sellas Tetteh naye anasubiri kuona kama timu yake ya Sierra Leone kama itafuzu Afcon au la. Ikishindwa, ndiyo anaweza kutua nchini na kujiunga na Simba.

Suala hilo, linawafanya Simba waone muda unasonga kwa kuwa tayari kocha aliyekuwa chaguo lao la kwanza, Kalisto Pasuwa wa Zimbabwe naye alibadili uamuzi wa kujiunga nayo baada ya kuiwezesha Zimbabwe kufuzu Afcon.

TETTEH
Simba wamekaa na wanaona chaguo lao la tatu, Joseph Omog raia wa Cameroon anaweza kuwa msaada mkubwa, hivyo wamalizane naye kabisa kimkataba.

Uamuzi wa Tetteh ulionekana kuwagawa Simba, wengine wakitaka asubiriwe. Lakini wengine wakiona muda unakwenda matiti.

Hivyo, leo Simba inaweza kufanya uamuzi wa mwisho kuhusiana na Omog ingawa wengi wanaona hakuna haja ya kufikiri sana kwa kuwa Omog anaijua Tanzania na aliipa Azam FC ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza na mwisho hadi sasa mwaka 2014.


1 COMMENTS:

  1. Download nyimbo mpya hapa ===>>http://www.hasheemjunior.com/

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV