June 22, 2016

CHIRWA

SIKU chache baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga, uongozi wa Yanga umemkabidhi jezi namba saba mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa.

Chirwa alitua nchini wiki iliyopita akitokea FC Platinum ya Zimbabwe aliyokuwa anaichezea pamoja na mshambuliaji tegemeo, Donald Ngoma.

Mzambia huyo, alisaini kuichezea Yanga akichukua nafasi ya Mniger, Issoufou Aboubacar aliyesitishiwa mkataba wake wa kuendelea kukipiga Jangwani hivi karibuni.

COUTINHO
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema jezi iliyobaki ni namba saba iliyokuwa inavaliwa na Mbrazili, Andrey Coutihno.

Saleh alisema, jezi hiyo huenda akaanza kuonekana akiivaa mechi na Mazembe itakayochezwa Jumanne  ijayo mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Chirwa tumempatia jezi namba saba iliyokuwa ikivaliwa na Coutinho, jezi ambayo haina mtu kwa hivi sasa tangu ameondoka Mbrazili huyo.

"Hivyo jezi ataanza kuonekana akiivaa kwa kuanzia mechi na Mazembe na nyingine zote zitakazofuata za michuano ya kimataifa,"alisema Saleh.


Chirwa akiwa anaichezea Platinum, alikuwa anaivaa jezi namba 9 inayovaliwa hivi sasa na beki raia wa Togo, Vincent Bossou.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic