June 16, 2016


Timu ya Nyangumi FC, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika michuano ya Umoja Cup dhidi ya wapinzani wao, Home Boys, inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Simba, Idd Selemani Meya.

Bao hilo pekee la Nyangumi kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tandale, jijini Dar es Salaam liliwekwa kimyani dakika ya 38 na mchezaji wao, Everest Bernard ambaye anaichezea Toto Africans ya Mwanza.Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, Meya alisema; “Nimekubaliana na matokeo na maamuzi yote ya waamuzi, ila vijana wangu wamejitahidi sama kwa kupambana lakini kosa moja tulilolifanya limetugharimu.”

Michuano hiyo imekuwa ikizidi kupata umaarufu kutokana na kasi ya kujulikana kutokana na ushindani unaozikutanisha timu husika. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV