June 26, 2016Kikosi cha Yanga kimetua nchini tayari kuwavaa wapinzani wao TP Mazembe na Kocha Hans van der Pluijm amesema vijana wake wako tayari.

Yanga imewasili kwa mafungu baada ya kundi la kwanza kutangulia na hilo la pili kutua usiku wa kuamkia leo.
“Kwa mazoezi tuliyofanya, marekebisho ya makosa ambayo tuliyaona baada ya mechi huko Algeria, tunaamini tuko tayari.

“Tunajua TP Mazembe ni timu kubwa, lakini tunataka kupambana na kufanya vema,” alisema Pluijm ambaye kikosi chake kiliwasili kwa mafungu.

Yanga inatarajia kushuka dimbani keshokutwa Jumanne kuwavaa Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV