June 2, 2016


Shabiki wa kugalagala wa Yanga, Ridhiwani Kikwete amesema amejitokeza kusema wazi iwapo Yusuf Manji atachukua fomu kugombea tena nafasi ya mwenyekiti, yeye atakuwa kati ya watakaompa kura.

Ridhiwani ambaye ni Mbunge wa Chalinze (CCM), amesema ameridhishwa na mafanikio iliyoyapata Yanga ikiwa chini ya Manji.

“Niwe mkweli kabisa Yanga imekuwa na maendeleo mazuri chini ya uongozi wa bwana Manji. Hili linanifanya kura yangu iwe kwake kama ataamua kuendelea kugombea,” alisema Ridhwani.


Manji anatarajia kuchukua fomu leo katika uchaguzi ambao utafanyika Juni 11 jijini Dar es Salaam.  

3 COMMENTS:

 1. Nakuunga mkono Riz one,tumpe Manji aongoze tena YANGA.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hilo si suala la hiari,asipopewa Manji unadhani kuna mwingine anayeweza kuiongoza yanga?Yanga ipo hapo ilipo kwa sababu ya fedha za Manji.Fedha ya Manji ndiyo inayoifanya Yanga ionekane bora,ni Manji anayesajiri na kuirndesha timu,asipochaguliwa utakuwa ni mwanzo wa mkwamo na tambo za wakimataifa,hata "Girl mulo" anafahamu hili.

   Delete
  2. Haha nimecheka sana hii comment. Na huu ndio ukweli yanga ni manji...hakuna yanga bila manji...hata "girl mulo" anatambua hatima ya mulo wake ipo mikononi mwa manji

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV