June 18, 2016


Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage ameibuka na kuwataka Simba kuandika barua ya kumthinisha beki Hassan Kessy ili kesho acheze.


Yanga iko Algeria tayari kuivaa Mo Bejaia katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, kesho. Kessy anakuwa tegemeo kwa kuwa beki Juma Abdul ni majeruhi.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf), tayari limeweka msisitizo kwamba Kessy na wachezaji wengine waliosajiliwa Yanga kama Andrew Vicent ‘Dante’ kutoka Mtibwa Sugar, Juma Mahadhi (Coastal Union) na Beno Kakolaki (Prisons) wanatakiwa kuwa na barua ya “kuwaachia”.

Rage amesema: “Yanga wanapaswa kuwa makini sana katika suala hili, la sivyo watakuwa wamepoteza nguvu zao bure.

“Kikubwa kama ikitokea wanahitaji ushirikiano kutoka kwa Simba, basi wafanye hivyo mara moja maana hapa sasa ni suala la utaifa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV