June 6, 2016

KAKOLANYA AKIWA NA KIKOSI CHA PRISONS

Kitendo cha Yanga kufanikisha usajili wa kipa Beno Kakolanya, kumezua gumzo kubwa kuhusiana na makipa wawili, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’.

Gumzo hilo limesambaa mitandaoni baada ya Yanga kukamilisha usajili wa Kakolanya kutoka Prisons.

Badaa ya Yanga kukamilisha usajili huo, mashabiki wapenda soka wamekuwa wakijadili kwamba Yanga haikuwa na pengo la makipa.

Wengine wanaamini Yanga kumsajili Kakolanya ni sawa na kuua kipaji cha kipa mmoja kwa kuwa ni rahisi wawili kupata nafasi na mmoja akaendelea ‘kuozea’ benchi.

Hata hivyo, taarifa kutoka Yanga zinaeleza, Kocha Hans van Der Pluijm amemtaka Kakolanya ili kuimarisha sehemu ya makipa.


Anaamini kuwa Yanga itakuwa na mechi nyingi mfululizo na Kakolanya atakuwa msaada mkubwa katika nafasi hiyo muhimu katika kikosi.

2 COMMENTS:

  1. Ukiangalia kakolanya ndo kipa mfup katka makipa wote waliopo pale yanga ...bnafc bado coni nafac ya kucheza kwake

    ReplyDelete
  2. Ukiangalia kakolanya ndo kipa mfup katka makipa wote waliopo pale yanga ...bnafc bado coni nafac ya kucheza kwake

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV