June 6, 2016


Uongozi wa Yanga umefanikiwa kukabidhi barua na viambatanishi inavyoamini ni sehemu ya hujuma kwa uongozi huo chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji.

Mkuu wa Habari na Mawasiliano ambaye ni Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amekabidhi barua na viambatanishi zikiwemo sauti ambazo zinatuhumiwa kuwa za aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Alloyce Komba.

Muro alikabidhi vitu hivyo katika makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) Upanga jijini Dar es Salaam.


Takukuru wameahidi kuviingiza kwenye uchunguzi na kuvifanyia kazi na watatoa taarifa uchunguzi wao utakapokamilika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV