Bondia Thomas Mashali naye amekuwa na mbwembwe kama yule bondia wa Marekani, Floyd Mayweather.
Hivi karibuni, Mashali alionekana akiwa amelala kitandani amepanga dola angalau chache.
Lakini safari hii, amepiga picha akiwa amefungua mdomo akionyesha meno ya dhahabu. Pia ana hereni na mkufu wa dhahabu.
Hii ni sehemu ya muendelezo kuonyesha kiasi gani ana fedha za kutosha na anaweza kujidai kwa fedha anazovuna.
0 COMMENTS:
Post a Comment