July 19, 2016


Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametamba kwamba atarejea dimbani akiwa imara maradufu.

Ronaldo amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goto mara kwa mara. Lakini aliingia katika michuano ya Euro 2016 akiwa fiti kabla ya kuumia tena baada ya kugonjwa na Dmitr Payet katika mechi ya fainali dhidi ya Ufaransa.

“Nawapongeza na kuwashukuru mashabiki wangu wote, lakini nawaambia nitarejea kwa kasi ya aina yake nikiwa imara zaidi,” aliandika Ronaldo kwenye mtandao wa kijamii.

Sasa Ronaldo raia wa Ureno amekuwa akiuguza majeruhi hayo huku kikosi chake cha Real Madrid kikiwa imeanza maandalizi.


Kwa mujibu wa Real Madrid, Ronaldo  hatacheza mechi ya Uefa Super Cup dhidi Sevilla Agosti 9 na anatarajia kukosa mechi tatu za mwanzo za msimu wa La Liga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV