July 29, 2016


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imeamua kutosaini mkataba wa kuendelea kuidhamini Simba.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza TBL imegoma kusaini mkataba ikionekana kuingia hofu baada ya Yanga kutotaka kuendelea nao au waingie wakiwa na ofa mpya.

“TBL wameona Yanga wanataka vitu vingi sana na kwao haitakuwa na faida, hivyo wameachana nao.

“Simba hawana shida, lakini watasaini vipi na Simba wakati kawaida zinatakiwa timu zote,” kilieleza chanzo.
“Hivyo wameamua kujiondoa na mkataba wao unaisha keshokutwa Jumapili.


“Sasa hili ni tatizo katika ulipaji mishahara kwa Simba maana lazima ugumu utaongezeka,” kilisisitiza chanzo.

Pamona na hivyo imeelezwa kumekuwa na juhudi binafsi zinazofanywa na baadhi ya viongozi kujaribu kuwashawishi TBL kupitia Kilimanjaro, wabadili uamuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV