July 19, 2016



Mashabiki wengi wa soka wameonekana kushitushwa na mwili wa beki wa Azam FC, Shomari Kapombe kuonekana umeongezeka sana.


Pamoja na mwili kuwa ni ‘bonge’, lakini bado amekuwa na mwonekano tofauti kutokana na kuwa na ndevu nyingi kama waigizaji wa filamu za Kihindi hasa wanapokuwa na mawazo au wametoka jela.


Hata hivyo, Kapombe ameanza mazoezi maalum chini ya kocha  wa viungo ambaye yupo katika jopo la Makocha wa Kihispania.

Kapombe alifanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini wiki kadhaa zilizopita na amekuwa akiendelea na matibabu.

Beki huyo aliyewahi kucheza nchini Ufaransa, alionyesha kiwango cha juu msimu uliopita ikiwa ni pamoja na kufunga mabao nane na kuwazidi washambuliaji wa timu nyingi za Ligi Kuu Bara.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic