July 20, 2016


Timu ya soka ya Ruvu Shooting ya mkoani hapa imeachana na kocha wake Tom Olaba raia wa Kenya licha ya kukirudisha Ligi Kuu Bara kikosi hicho.

Badala yake, mikoba ya Olaba sasa amekabidhiwa kocha mzawa Selemani Mtingwe aliyemaliza mafunzo ya ukocha ya leseni daraja B hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, Olaba na timu hiyo wameamua kuchana na sasa watakuwa na Mtingwe aliyekuwa kocha msaidizi.

“Ruvu Shooting tunaheshimu sana mchango wa Olaba katika timu yetu na tunamheshimu sana Olaba, tutaendelea kumheshimu na kuamini kuwa ni miongoni mwa makocha bora katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu na Afrika.

“Uongozi wa Ruvu Shooting chini ya Mwenyekiti wake Kanali Charles Mbuge tunamtakia kila la kheri Olaba, kocha makini, mahili, mcheshi, mwenye weledi na akili nyingi katika kufundisha soka.

“Ruvu Shooting tunamkumbuka, tutaendelea kumkumbuka kwa mema na mafanikio makubwa ndani ya timu yetu chini ya uongozi wake,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Bwire.
Olaba alijiunga na Ruvu Shooting msimu wa mwaka 2013/14 mzunguko wa pili baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu Boniphace Mkwasa kuvunja mkataba na kujiunga na Yanga. 

Msimu wa 2014/15 Ruvu Shooting ilishuka daraja chini ya Olaba lakini amefanikiwa kuirudisha ligi kuu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic