July 6, 2016Beki kisiki mpya wa Yanga, Andrew Vicente 'Dante' ametangaza kugomea jezi namba 28 anayoitumia kwa sasa kwenye michuano ya kimataifa na kueleza kuwa anataka kutumia jezi namba mbili kwenye ligi kuu msimu ujao kwa kuwa haina mtu baada ya Salum Telela kutemwa.

Dante anasema ataomba kupatiwa jezi hiyo kwani ndiyo ya bahati maishani mwake, lakini pia anatamani kuipata namba 12, aliyokuwa akiitumia Mtibwa Sugar ambayo kwa Yanga inavaliwa na Juma Abdul huku 23 ikitumiwa na nahodha wa kikosi hicho Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Iwapo ombi lake litakubaliwa, Dante ataungana na Amissi Tambwe ambaye msimu uliopita alitumia jezi mbili tofauti. Katika ligi kuu alitumia namba 19 huku kimataifa akitumia namba 29 kutokana na kile kilichotajwa 'walijichanganya' kwenye utumaji majina Caf.

Dante alisema alikubali kuitumia No.28 kwa kuwa walikuwa kwenye michuano ya kimataifa, pia jezi yake ilikuwa na mtu.


"Kama watanikubalia, nitachukua namba mbili kwenye ligi kuu msimu ujao. Naipenda na ndiyo namba yangu tangu enzi na enzi lakini wakisema ameshapewa mwingine, poa nitavaa yoyote. Pia zipo ambazo ninapenda kama 23 angalia ndiyo ya nahodha (Cannavaro) na 12 yupo Abdul ndiyo maana nitajaribu kuwaambia hiyo namba mbili," alisema beki huyo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV