July 5, 2016


MANARA
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara, amepata matatizo kwa kuwa amepoteza uwezo wa kuona baada ya jicho lake moja kushindwa kuona.

Manara ambaye ni mcheshi anatumia jicho moja la upande wa kulia.

Akizungumza na SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, leo Manara amesema:

“Ni kweli nimepata tatizo, jicho la upande wa kushoto halioni na sijui sababu ni nini.

“Nimenichanganya sana, tayari nimeanza matibabu. Nimechukua vipimo katika hospitali kadhaa, hivyo siwezi kusema hali yangu ni nafuu, mbaya au nzuri hadi nitakapopata majibu.

“Yeyote anayejua sehemu ambayo ninaweza kupata tiba bora kuhusiana na suala hili anaweza akanisaidia tafadhari,” alisema Manara.


SALEHJEMBE, INATOA POLE MANARA NA KUMTAKIA NAFUU MUNGU AMSAIDIE APONE HARAKA.

1 COMMENTS:

  1. Saleh hiyo ndio Exclusive ambayo umefanya na manara? We si n mhariri kabisa, jifunze kuandika stori vizuri na unaposema kitu exclusive kwetu sisi wenye uwezo wa kufikilia kwa mapana tunaelewa ni more stori, hata kama sio feature stori

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV