July 5, 2016


Pamoja na kusumbuliwa na enka, kiungo mpya wa Yanga, Juma Mahadhi amesema ana matumaini atarejea.

Mahadhi amekuwa akifanya mazoezi ya taratibu chini ya uangalizi wa daktari wakati wenzake wakiendelea na mazoezi ya kawaida na magumu.

“Naendelea vizuri, nina matumaini nitapona kabisa,” alisema Mahadhi ambaye alionekana ni mtulivu.

Wachezaji wengine waliendelea na mazoezi kama kawaida chini ya Kocha Hans van der Pluijm.

Inaonekana ubabe wa mabeki wa TP Mazembe hasa yule aliyemkanyanga ndiyo limekuwa tatizo kwa Mahadhi ambaye amejiunga na Yanga akitokea Coastal Union.


Madhadhi anaonekana kuwa hazina ya baadaye ya Tanzania kwa kuwa umri mdogo na anaonyesha kuwa na kipaji hasa kama atajitunza na kutaka kujiendeleza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV