July 2, 2016Kikosi cha Wales, kuanzia kocha Chris Coleman, wachezaji na mashabiki wan a furaha kubwa kuwatwanga masupastaa wa Ubelgiji kwa mabao 3-1 na kuushangaza ulimwengu kwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Euro 2016.

Lakini hakuna anayeweza kusahau bao la pili la Wales lililofungwa na Hal Robson-Kanu.

Kanu alipokea mpira akiwa katikati ya mabeki watatu wa Wales, akaumiliki mpira, akausogeza katikati na kugeuka kabla ya kufunga vizuri na kwa ufundi wa juu kabisa.

Bao hilo, hadi sasa linaonekana kuwa ndiyo bora zaidi kuliko mengine yaliyofungwa katika michuano ya Euro.


Inawezekana ukawa na maoni tofauti, basi tupe bao unaloona ndiyo bora zaidi kama si hili la Hal Robson-Kanu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV