July 17, 2016


Mashabiki mbalimbali wa soka, wamemshambulia kwa maneno makali beki wa Yanga, Haji Mwinyi baada ya yeye kuweka picha yake mtandaoni kupitia ukurasa wake wa Facebook na kuandika “Wengine mtanipenda nikiondokaga”.

Katika picha hiyo, anaonekana akiwa na kiungo mwingine kinda wa Yanga, Juma Said 'Makapu' lakini baadhi ya mashabiki waliomuandikia mtandaoni wanaonekana kutomjua na kumuita "masela wako".

Wengi waliochangia walionekana kumlaumu kwamba Yanga haijafanya vizuri katika mechi ya jana dhidi ya Medeama lakini yeye anaweka picha za furaha.

Wengine wanaonekana kumshauri vizuri na baadhi wamemshambulia hali inayoonyesha kutofurahishwa na kitendo chake hichio.

Wakati anatua Yanga, Haji Mwinyi alianza vizuri lakini kiwango chake kimekuwa kikiporomoka kila kukicha.

Baadhi ya mashabiki wamemshauri “kukaza” ili kukirejesha kiwango chake huku wakimsisitiza kuhusiana na suala la nidhamu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV