MANARA ALIPOKUTANA NA FOWADI ELIUS MAGURU, UWANJA WA NDEGE WOTE WAKIWA SAFARINI. |
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara ameanza kufanyiwa vipimo vya macho yake nchini New Delhi nchini India.
Manara yuko India kwa ajili ya vipimo hivyo baada ya jicho lake moja kupoteza uwezo wa kuona na jingine kupunguza uwezo wa kuona hadi asilimia 10 tu.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MWIGULU NCHEMBA AKIWA PAMOJA NA MANARA NA FAMILIA YAKE ALIPOFIKA KWAKE MAGOMENI MIKUMI JIJINI DAR ES SALAAM KUMJULIA HALI. |
Lakini tayari kazi ya kumchukua vipimo imeanza na huenda matibabu yakaanza ndani ya simu mbili.
Leo asubuhi, Manara amezungumza na SALEHJEMBE akiwa jijini New Delhi na kusema: “Nimeanza vipimo.”
SALEHJEMBE, inamtakia Manara kila la kheri na afanikiwe katika matibabu yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment