July 2, 2016


Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ leo Jumamosi inacheza na Shelisheli mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Madagascar.

Mchezo huo unachezwa huku Serengeti Boys ikiwa na faida ya ushindi wa kwanza wa mabao 3-0 iliyoupata wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime ameliambia Championi Jumamosi: “Vijana wangu wapo vizuri hakuna mgonjwa hivyo ni matumaini yangu kuwa tutafanya vizuri kama ilivyokuwa nyumbani katika mchezo wa kwanza.”

Endapo Serengeti Boys itafanikiwa kuitupa Shelisheli nje ya michuano hiyo, hatua inayofuatia itapambana na Afrika Kusini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV