Msemaji wa Simba, Haji Manara ameondoka nchini usiku wa kuamkia leo kwenda India kwa ajili ya matibabu ya macho.
Wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Manara amekutana na mshambuliaji Elius Maguri ambaye sasa anakwenda kuanza rasmi kazi nchini Oman.
Manara na Maguri walijumuika pamoja kwa ajili ya safari hiyo.
Manara anakwenda kutibiwa baada ya jicho lake moja kupoteza uwezo wa kuona huku jingine likiwa limepungua kabisa uwezo.
Matibabu rasmi yanatarajiwa kuanza kesho Jumanne kwa kuchukuliwa vipimo.
0 COMMENTS:
Post a Comment