July 13, 2016


HERNANDEZ (KULIA) AKIWA NA MMOJA WASAIDIZI WAKE

Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez raia wa Hispania ameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpatia mechi moja ya kirafiki.

Uongozi nao umemjibu kwa kumpa mechi dhidi ya Ashanti United ili apate nafasi ya kuwaona wachezaji wake ambao amekuwa akiwafanyia majaribio.


Kocha huyo amekuwa akiwafanyia majaribio wachezaji wapya na wale wa zamani akishirikiana na jopo la makocha wengine kutoka Hispani.

Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia na Msaidizi wake, Pablo Borges na Kocha wa Makipa Jose Garcia na Daktari wa timu, Sergio Perez.


Kocha huyo alitoa siku 15 za maandalizi na kuwaangalia wachezaji wapya na wa zamani na baada ya hapo atakuwa na jibu wapi wanaotakiwa kusajiliwa na wachezaji gani wanaopaswa kuachwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV