July 13, 2016


Wanachama na mashabiki wa Yanga, usiku huu wametua nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara eneo la Magomeni Mikumu jijini Dar es Salaam na kukabidhi mchango wao kwa ajili aya matibabu.

Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro na walimkabidhi Manara kiasi ya Sh 1,055,000 kama mchango wao.


Wiki iliyopita, Manara aliamka jicho la kushoto halioni. Pia jicho lake la kushoto halioni vizuri pia. Hivyo anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu na safari yake huenda ikawa Jumamosi hii.

Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga.

“Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini ni mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.

“Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga wanazika Simba, Yanga wanazika Simba. Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV