July 13, 2016


TELELA

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo Julio, amesema tayari amewasiliana na Salum Telela na kumueleza nia yake ya kumsajili Yanga.

Julio amesema baada ya kuzungumza na Telela, anamuachia nafasi ya yeye kutafakari kuhusiana na uamuzi wa kujiunga na Mwadui FC baada ya kuachwa na Yanga.

JULIO
“Suala la ndiyo au hapana ninamuachia yeye. Kawaida ni mtu wa uwazi, namueleza mtu nia yangu baada ya hapo ninamuacha aamue,” alisema Julio.

Hivi karibuni, baada ya Yanga kumtosa, Telela alitangaza kupumzika na mambo ya soka na badala yake kujiendeleza zaidi kimasomo.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV