July 5, 2016

OMOG
Kocha Joseph Omog wa Simba, ameweka msisitizo kwa kikosi chake kuanza mazoezi bila ya kuwa na rundo la mashabiki.

Omog ambaye aliuambia uongozi angetaka mazoezi yasiyo na mashabiki wengi ili wachezaji wawe huru naye aweze kuwaona, amesisitiza hilo tena.

Simba ilikuwa ianze mazoezi jana, lakini ikakosa uwanja ambao ungeendana na anachotaka Omog.

"Kweli kocha anataka uwanja ambao atakuwa yeye na wachezaji wake, anataka wawe huru, wacheze wakijiachia na yeye apate nafasi ya kung'amua anayotaka," alieleza mmoja wa viongozi wa Simba walio katika kamati ya utendaji.

Pamoja na kuzuia mashabiki, Omog alizuia kikosi chake kuanzia gym kama ilivyozoeleka, badala yake akataka wachezaji kuanza na mazoezi ya uwanjani na hasa kucheza mpira kwanza na baadaye ataingia kwenye programu ya gym.

Raia huyo wa Cameroon aliyewahi kuipa Azam FC ubingwa wa Ligi Kuu Bara mwala 2014, ndiye kocha mpya wa Simba na atakuwa akisaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV