July 5, 2016


Meneja wa beki Hassan Kessy ameuomba uongozi wa Simba, kuangalia zaidi kwa ajili ya suala la beki huyo ili apate nafasi ya kucheza.

Athumani Tippo amesema ana imani kubwa uongozi wa Simba unaweza kulimaliza na kuusisitiza uongozi wa Yanga, uwasiliane na ‘wenzao’ ili Kessy aanze kucheza.

“Nafikiri hili suala limekwenda ‘level’ ya klabu kwa klabu, ingawa tumelifikisha Sputanza kama sehemu ya process lakini naamini Simba na Yanga wanaweza kulimaliza hili.

“Ninawaimba walimalize ili huyu kijana aweze kuendeleza kipaji chake. Najua Simba hawamhitaji kwa sasa, hivyo wampe nafasi.

“Kama kuna sehemu wanaona alikosea, wanaweza kumuonya kama kijana wao halafu wakampa nafasi. Binadamu wanakosea mambo mengi sana na wanaweza kurekebishwa na kundelea na maisha,” alisisitiza Tippo.

Kessy amesaini mkataba Yanga lakini wakati anasaini mkataba wake na Simba ulikuwa umebaki siku chache jambo ambalo Simba wanalishikilia.

Lakini imeelezwa kwamba viongozi wa Simba wamekuwa na hasira na Kessy kwa kuwa ‘aliwasaliti’ huku akionyesha wakati anaondoka hasa katika mechi za mwisho wa ligi.

shambuliaji wa Yanga Obey Chirwa natarajia kurejea nchini ndani ya siku chache akitokea kwao Zambia.

Mmoja wa rafiki zake wa karibu, amesema matatizo yaliyompeleka Zambia ameyafanyia kazi na atarejea ndani ya siku chache.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV