July 5, 2016


Kipa wa zamani wa Tenerife ya Hispania, Juan Jesus Gonzalez amesema yuko tayari kwa ushindani licha ya kwamba ni mara yake ya kwanza kucheza barani Afrika.

Jesus yuko nchini kwa ajili ya kufanya majaribio ili ajiunge na Azam FC kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza leo na SALEHJEMBE, Jesus amesema matarajio ya ushindani mkubwa ni jambo jema kwake.

"Nataka kushindana na kufanya vizuri, najua Azam ni timu kubwa Tanzania. Nitaonyesha uwezo wangu," alisema akionyesha kujiamini.

Kipa huyo mtaratibu, ametua nchini tayari kwa ajili ya kujiunga na Azam FC kama watakubaliana na uongozi wa klabu hiyo ambayo ndiyo mpinzani mkubwa wa watani Yanga na Simba.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV