July 11, 2016

Malaria ni ugonjwa hatari aisee. Mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe amejikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kuumwa malaria.

Hadi leo, Tambwe raia wa Burundi ametundikwa jumla ya drip sita ili kuhakikisha anapata nafuu.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Tambwe amesema ametoka hospitali na sasa anaendelea vizuri, tofauti na ilivyokuwa siku mbili zilizopita.


“Sasa naendelea vizuri, lakini nilikuwa nina malaria kali,” alisema Tambwe ambaye yuko kwenye kambi ya Yanga inayojiandaa kucheza na Medeama ya Ghana katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV