July 29, 2016


Kocha msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ametamka kuwa sasa tayari wameshapata ‘first eleven’ ya kikosi hicho ambacho wana imani kuwa itasumbua kwenye ligi kwa msimu ujao.

MAYANJA
Mayanja kwa sasa yupo pamoja na kocha mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog mkoani Morogoro wakiendelea na programu zao kwa ajili ya kukiweka sawa kikosi hicho kabla ya ligi kuanza.

Mayanja amesema kuwa tayari wana orodha kamili ya kikosi hicho ambacho kimepatikana baada ya kuwaangalia nyota wote waliopo klabuni hapo ambapo ripoti kamili wanatarajia kuiwasilisha kwa viongozi mwisho wa mwezi huu.

“Tayari tuna majina ya wachezaji ambao wataanza kwenye kikosi cha kwanza ambapo hapo tumeangalia viwango vya wachezaji wote kabla ya kuwateua na kuwaingiza kwenye timu hii.


“Ripoti ya kikosi kizima tunatarajia kuwapa viongozi mwishoni mwa mwezi huu ambapo tunaamini kwa kupitia first eleven hii, wapinzani wetu wajiandae vema,” alisema Mayanja.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV