July 6, 2016

MORAD
Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu Azam FC iachane na beki wake wa kati, Said Morad, imebainika kuwa timu ya Mbeya City imetia mkono kumwania mchezaji huyo kwa ajili ya msimu ujao.

Mtu wa ndani kutoka Mbeya City amesema kuwa timu hiyo imeshaanza kuzungumza na mchezaji huyo wa zamani wa Ashanti United na Simba SC ingawa bado hawajafikia kwenye suala la kuelewana ada ya usajili.

“Kwanza ilikuwa ni kufahamu kama yupo tayari (Morad) kwa mazungumzo na kuja kucheza Mbeya msimu ujao kisha mengine yatafuata kama dau la usajili analolitaka na vitu vingine vya kimkataba zaidi, kwa hiyo bado kuna harakati zinaendelea,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Morad kuzungumzia suala hilo, alisema: “Wao walinicheki, tukazungumza kidogo, kuhusu vitu vingine wakitafutwa wao ndiyo wanaweza kufafanua vizuri zaidi.”

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema: “Kulikuwa na mpango huo wa kuzungumza na Morad lakini baada ya kusikia amekwenda Simba ikabidi tusitishe lakini kumbe haikuwa hivyo, kwa hiyo tutaangalia itakuwaje.”


Jumapili iliyopita kuliibuka kwa taarifa za Morad kusajiliwa na Simba lakini baadaye siku hiyo mchezaji huyo akaibuka na kukanusha vikali juu ya kuzungumza au kufikia makubaliano yoyote na Wekundu hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV