July 6, 2016

KASEKE (KULIA)...
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke jana alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya jijini Dar.

Kaseke ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mbeya City alipata ajali hiyo akiwa amepanda pikipiki asubuhi wakati akiwahi mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Medeama ya Ghana kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Julai 15, mwaka huu.

Timu hiyo, tayari imepoteza michezo yake miwili hadi hivi sasa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe ambayo kila mmoja walifungwa bao 1-0.
Championi Jumatano, ambalo lilikuwa kwenye mazoezi ya Yanga jana, lilimshuhudia kiungo huyo akiwa nje ya uwanja akishindwa kufanya mazoezi na wenzake kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata mwilini mwake.

Daktari mkuu wa timu hiyo, Edward Bavo, alisema beki huyo ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake kutokana na maumivu na majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali ya bodaboda.

Bavo alisema, kiungo huyo alipata ajali hiyo asubuhi ya jana maeneo ya Ubungo wakati akiwa anakwenda mazoezi Boko.

"Kaseke ameshindwa kufanya mazoezi baada ya kupata ajali ya bodaboda iliyomsababishia michubuko kwenye magoti na sehemu nyingine za mwili wake.


"Ajali hiyo aliipata maeneo ya Ubungo akiwa anatokea kwake Kimara anapokaa, hivyo uongozi umemuwahisha hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi,"alisema Bavo.

1 COMMENTS:

  1. Du wakimatifa wanapanda Bodaboda badala ya ndege!! Pole dogo, upone haraka!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV